TAFITI ZITUMIKE KUONDOA CHANGAMOTO KATIKA JAMII. DC kizigo Mpwapwa.
Na Mwandishi wetu.Mpwapwa.
Serikali imeobwa kuzitumia tafiti mbalimbali zinazofanywa na tasisi mbaliimbali hapa nchini Katika kupata majawabu ya changamoto zinaikabili Jamii yetu Kwa Sasa .
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia kizigo akihutubia muhadhara katika Uzinduzi wa Utafiti uliofanya na shirika la RELI.
Katika utafati uliofanywa katika wilaya ya Mpwapwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la RELI ambalo liliangazia Katika masuala ya kiwango cha uelewa wavijana Katika viwango mbalimbali ambapo utaffiti ulibaini kati ya vijana 10 ni vijana wanne waliweza kuwa na uelewa wa kiwango cha Moja cha utatuzi wa changamoto amabacho ni kiwango cha chini kabisa.
Katika masuala ya kujitambua utafiti ulibaini asilimia kubwa ya vijana walionekana Kati ya vijana 10 ni vijana 5 walionekana kujitambua na Katika suala la heshima ilibainisha asilimia 49.9% ya vijana Wana heshima.
Aidha utafiti huo ulilenga kuanzia masuala makuu mnne ambayo ilikuwa ni kuangalia ulewa wa vijana Katika kujitambua ,ushirikiano,utatuzi wa matatizo na kiwango cha heshima Kwa Jamii.
Alisema Katika kiwango cha heshima vijana wengi wana uelewa wa kati Katika kuheshimiana.
Akifungua utafiti huo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo Alisema Nchi zote zilizoendelea zimetumia tafiti mbalimbali Katika kuondoa CHANGAMOTO za Jamii.
Hata hivyo alidai kuwa serikali imekuwaikitumia tafiti zinazofanywa na tasisi zisizo kuwa za kiserikali.
Comments
Post a Comment