MADWANI MPWAPWA WALIA NA SHERIA ZA MADINI.
BARAZA la madiwani katika halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa limeiomba ofisi ya ofisa madini mkazi Dodoma kuweza kuwajengea uwezo madiwani hao na wadau wanaofanya kazi za madini katika halmashauri hiyo ikiwa ni mkakati wa kukuza mapato ya ndani ya halmasahauri hiyo. Akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya fedha uongozi na mipango katika kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2017 diwani wa kata ya Lumuma bwana Jocktan Cheliga amesema kuwa pamoja na wilaya ya Mpwapwa kuzungukwa na neema ya madini ya aina tofauti tofauti lakini wameshidwa kufaidika na rasilimali hiyo kutokana na madiwani wengi kuto kujua taratibu za upatikanaji wa mirahaba ya madini katika maeneo husika. Diwani wa kata ya Mazae bwana wiliamu Vahae akichangia mjadala katika kikao cha madiwani Mpwapwa. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Donart Ngwezi amesema kuwa lazima kuwepo na ushirikiano wa pamoja kati...