Mpango wa PWP TASSAF MPWAPWA UTASAIDIAMAZINGIRA
Imeelezwa kuwa
shughuli za ajira muda
zilizofanywa na walegwa wa mpango wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu kama
kutunza Misitu ya asili,uvunaji wa maji ya mvua, na utunzaji wa udongo,ikitumika
inavyopaswa itaweza kuleta mabadiliko
chanya kwa jamii na kuweza kujiletea maendeleo endelevu.
Kauli hiyo ilitolewa na
Mratibu wa Tassaf wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Paskal Jeremia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu
tadhimini ya utekelezaji wa mpango wa
ajira za muda zijulikanozo kama (PWP)kwa wanufaika wa mpango huo wilayani hapa
Jeremia alisema rasilimali hizo kama ujengaji wa miundo mbinu
ya kuvuna maji ya mvua, wa utunzaji wa misitu, na uhifadhi wa
udongo ngazi ya jamii italeta mabadiliko kuwa mazuri zaidi
na jamii kuweza kujiletea
maendelea endelevu katika maeneo yao yanayoishi .
Aidha alisema kwa sasa zoezi hilo limetekelezwa kwa
zaidi ya asilimia 70% katika vijiji vyote
ambavyo mradi huo ulitekelezwa
bali alisema kuna baadhi ya changamotozilizojitokeza kama za malipo ambazo
makao makuu yanazifanyia kazi na walegwa watalipwa muda si mrefu.
Alisema
Mpango wa Tassaf katika awamu
zote tatu umeweza kuonyesha mafanikio
mazuri ngazi ya jamii na halmashauri
kwa walegwa walioko kwenye mpango wameweza kubadilisha maisha yao kwa kujiibulia miradai
midogomidogo na kuweza kumubudu maisha yao ya kila siku.
Hata hivyo alisema
mapango huo tangu uanzishwe japo
kuwa umeongeza ajira lakini pia umeweza
kupunguza kiwango cha umaskini ngazi ya jamii na kusaidia kufikia
malengo ya Mkukuta
pamoja na kufikia malengo ya mileniam
ya kukuza kipato cha kaya mojamoja.
Pia alisema katika wilaya
ya Mpwapwa ni na jumla ya wakazi 6,048 wananufaika na Mpango wa kaya maskini
japo kuwa kuna zoezi la uhakiki wa walegwa hewa unaenelea katika kata zote za
mpango.
Kwa upande wake ofisa
ushauri naufuatiliaji wa Tassaf wilayani hapa bwana Hosea Sichone alisema madhumuni ya
mpango ni kuziwezesha kaya
maskini sana kuongeza matumizi muhimu
kwa jia endelevu na kuziwezesha kaya
hizo kuwa na pesa za matumizi wakati
kipindi kigumu zaidi.
Hata hivyo Hosea alisema
kuwa pia madhumuni mengine ni kuwekeza katika rasilimali watu hasa watoto ikiwa na lengo la kuaandaa kizazi
chenye tija ,kuimarisha shughuli za
kuongeza kipato na kuongeza shughuliza za huduma za jamii.
Mmmoja wawanufaika wa
Mpango huo Bi Maligalitha Chinoga alisema kama jamii itaweza kushilikishwa
vizuri na kuto kuingliwa na siasa zoezi hili litweza kuleta mafanikio makuu kwa
jamii.
Bi Chinoga aliongeza kuwa
miradi ya kutoa ajira za muda kwa
kaya maskini japo kuwa unalenga
katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali hewa lakini lakini uharibifu
mkubwa wa mazingira katika wilaya yetu unatishia uendelevu wa miradi hiyo.
Comments
Post a Comment