ASKOFU KINYAIA AWAASA WATANZANIA.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la
Dodoma Mhasahamu askofu Beatus Kinyaia
amewataka watanzania kuto kukubali kufa kizembe kwa kungangania mazoea
ya kuto kupanda mazao yanayostahimili ukame katika kipondi hiki cha mabadiliko
ya Tabia ya hali ya hewa.
Askofu
alizungumza hayo jana jumapili ya januari Mosi 2017wakati wa misa katika Kanisa la Bikira maria
wa Fatima kanisa la hija katika
Parikia ya Mpwapwa .
Kinyaia
amesema haridhishwi na tabia ya baadhi ya watanzania wengi kuendelea kung’ang’ania mazoea ya kuto kukabiliana na ushauri wa
watalaam na maafisa kilimo kuwataka kupanda mazao yanayoweza kukomaa
mapema na yanayoweza kustahimili
ukame ili kuweza kupata tija ya kilimo
chao
Aidha Askofu Kinyaia
alisema “siku za hivi karibuni
mamlaka ya ya utabili wa hali ya
hewa imetangaza kuwa katika kipindi hiki cha
msimu wa mvua kutakuwa na mvua chini ya wastani hivyo kuwataka wananchi
kuweza kupanda mazao yanaweza kuhimili ukame
na kukomaa mapema kama Mtama , Uwele, Alizeti, na Muhogo”alisisitiza
Akofu Kinyaia.
Alisema ni lazima Watanzania katika mwaka
mpya 2017 hakutakuwa na mbadiliko ya mtu kama mtu mwenyewe hatakubali
kubadilika kifkra, na kimtazamo ,na kufanya
kazi kwa bidii kwa kujiletea
maendeleo yake binafsi na Taifa nzima.
Alisema kumekuwako na lindi la akina dada
kufanya biashara za ngono,uuzaji wamadawa ya kulevya , na biashara zote haramu
ambazo ni chukizo kwa Mungu na kwa jamii pia ambazo alisema kuwa ni watu wengi
kushidwa kujishughulisha kupenda tabia ya ubinafsi bila kujali matokeo ya kazi
wanazo zifanyakwa taifa na jamii nzima,
Hata hivyo
alisema kuwa katika baadhi ya
mikoa ya Dodoma haitaweza kuwa na njaa
kila mwaka endapo wakulima wao wakabadilika na
kulima kwa kufuata maelekezo ya
wataalamu na kuzingatia mabadiliko ya tabia
nchi na mabadiliko yatabia ya hali ya
hewa.
Kwa wake Paroko wa kanisa hilo Daud Ngimba
alisema katika ibada katika Misa
hiyo kutatolewa kipaimara kwa vijana
zaidi 278 ambao walipokelewa katika kanisa
na kuwa wafuasi wa Kristu walio
imarika.
Comments
Post a Comment