WANCHUO WAMTUMBUA MKUU WAO
SAKATA la la uwajibishwaji kwa la viongozi wazembe likiwa linashika kasi katika tasisi mbalimbali za umma na za serikali sasa limemkuta mkuu wa chuo cha wanannchi Chisalu bwana Sebastian Aweit kuvuliwa madaraka yake kwa muda na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa tuhuma mbalimbali. Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika chuo cha wananchi Chisalu kilichopo katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa bala baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa bwana Jabili shakimweli ambae ni mkuu wa wilaya hiyo kummvua madaraka ya ukuu wa chuo kwa muda, mkuu wa chuo cha maendeleo ya wananchi Chisalu Bwana Sebastian Aweit kwa kushidwa kuongoza chuo hicho . Shakimweli amesema amefikia uamuzi huo mala baada ya kuona na kujiridhisha juu za tuhuma zilizotolewa na wanachuo wa chuo hicho hadi kupelekea wanafunzi kugoma kuingia madarasani na kutish...