WAFANYA BIASHARA WAILALAMIKIA HALMASHAURI.
Na Stephen noel mpwapwa
UMOJA wa wafanya biashara wa
mazao na wakulima CHAWAMA wilayani
mpwapwa mkoani Dodoma wamelalamikia uongozi wa halmasshauri ya wilaya ya mpwapwa kwa upandisha ushuru wa mazao bila kuwashirikisha
wafanya wanaya biashara hao.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na ras
fm mjini hapa wamesema kuwa halmashauri
imewapandishia ushuru kutoka shilingi
1000 kwa gunia hadi shilingi 5000 kwa gunia kitu walichosema kuwa halmashauri inazidi kuwadidimiza zaidi.
Akiongea makamu mwenyekiti wa umoja
wa wafanya biashara za mazo(CHAWAMA) wilayani hapa Hamis Ally amesema
wameshitushwa na uongozi wa halmasahauari hiyo kupandisha ushuru wa
mazao bila kushirikiana na wadau, na
bila kuboresha huduma katika soko
hilo,zikiwemo huduma za vyoo, maji na umeme ambapo hulazimu kujisaidia
vichakani na kwenye majumba ya watu.
Aidha Stephano Luhanga mfanya biashara wa karanga
pia utaraibu wa utozaji wa ushuru kwa
mkulima umekuwa ni wa kinyonyaji ambapo
alisema gunia moja hutozwa zaidi ya mala mbili
mazao yanapotoka shambani, yanaposafirishwa na yanapouzwa pia hutozwa.
Luhunga amedai kuwa pamoja
na kubadilisha bei ya ushuru huo ambao halmashauri ilingia
mkataba na Kampuni ya ADOSTA Limited ya mjini Dar-es –salaam ambayo ilipewa mkataba wa mwaka mmoja lakini
kabla hawajamaliza mkataba kampuni hiyo imebadilisha bei za tozo za ushuru huo bila
kuwashirikisha wadua na mabaraza la madiwani.
Hata hivyo wafanya biasahara hao
walienda mbali na kuadai uongozi wa halmsahauri umekuwa ikitoa kazi kwa wageni
na kuwaacha wazawa kitu alichosema kina
pelekea wilaya hiyo kushidwa
kuendelea kwa miaka 31 sasa tangu
ianzishwe.
Pia wamesema kampuni hiyo ya
ADOSTA inajiamlia kufanya hivyo kutokana na ina ubia na kigogo mmoja wa
halmasahauri hiyo
Jackson Mwazigila amesema baadhi ya viongozi wa halmasahauri hiyo wameigeuza halmasahauri kama shamba la bibi
kwa kukusanya ushuru na huku huduma za jamii katika wilaya hii ikizidi
kudidimia kila kukicha.
Pia wamesema wakazi wa wilaya hiyo wakiomba kazi ya uzabuni au uwakala hawapewi hadi watoe rushwa ,kitu
walichosema ndicho chanzo kinacho changia halmasahauri hiyo kutishiakufa na kushidwa kujiendesha kwa
mapato yake ndani na hivyo hujiendesha kwa kutegemea fedha kutoka serikali kuu.
Ras fm aliamua kwenda kwa
mkurugenzi mtendaji wa halmasahauri kujua kinachoendelea na mkurugenzi aka jibu kuwa hajui chochote kutokana na kuto kuwepo ofisini kwa muda wa wiki tatu
sasa, na hivyo hawezi kuzungumzia kitu chochote hadi hapo alipo lazimishwa na
mwenyekiti wake wa halmashauri hiyo kutolea ufafanuzi wa suala hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri
ya wilaya ya mpwapwa Mwajina lipinga
alidai wameamua kulifanya hilo kwa muujibu wa sheria kuu ya biashara ya mwaka 1982 iliyo fanyiwa malekebisho
mwaka 2002.
Kauli ya mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri hiyo ilikinzana na kauli ya mwenyekiti wa halmasahauri ya
wilaya ambao ilimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kusitisha
ushuru huo na kutaka wafanya
biashara kuendelea kutozwa bei ya zaani ya shilingi 1000 kwa gunia kwa kile alichosema kuwa hapo
wafanya biashara hao watakapo elimishwa
na kufahamishwa zaidi juu ya tuzo hizo.
Comments
Post a Comment