KAZI KUBWA KUIONGOZA SERIKLI ILIYO JAA RUSHWA.ASKOFU MKUU ANGLIKANA TANZANIA
Na Stephen noel –mpwapwa
ASKOFU MKUU wa kanisa la Angilikana Tanzania Dr. Jacob Chimeledya amesema kuwa kuna gharama kubwa kutunza na kulinda
seriklai iliyo jaa vitendo vya rushwa na ufisadi kuwa vinaweza
kuhatarisha amani ya Nchi yetu.
Askofu chimeledya aliyasema hayo alipokuwa akihubiri katika ibada iliyofanyika katika kanisa kuu la watakatifu wote Vinghawe
mjini Mpwapwa.
Amesema kumekuwako na na vitendo vya vya
kuhatarisha amani ambayo husababishwa
na viongozi waliopewa nafasi na wananchi
wanyonge kwa kujimilikisha mali
za watanzania wanyonge kusababisha kuwepo kwa kundi kubwa la walionacho na wasio
nacho kitu alichosema kinasababishwa na ubinafsi kupungua kwa uadilifu na kutawala kwa rushwa ndani ya taifa letu.
Alisema vitendo vya ufisadi vinavyo endelea ndani ya serikali “vinasababishwa na watanzania
wanyonge wanakufa kwa kukosa dawa
hospitalini, akina mama wanakufa kwa kukosa vifaa vya kujifungulia,na watoto mashuleni
hawana vifaa vya kutosha mashuleni huku mtanzania mmoja namiliki pesa
ambazo zinaweza kupunguza
matatizo hayo”alisema Askofu Chimeledya .
Aidha alisema
kuwa “naipongeza tume ya katiba chini ya
kiongozi wake jaji msatafu Lubuva
kwa kuweza kuahirisha zoezi la upigaji kura hapo april 30 mwaka lingeweza
kulisababishia taifa hasara kubwa na
kutumia vibaya rasilimali za watanzania”aliongeza na kusisitiza
Chimeledya.
Amesema pamoja na kuahirisha
zoezi la kupigia kura katiba
pendekezwa aliitaka serikali kuweza
kurekemisha changamoto zote
zilizo jitokeza wakati wa uandikishaji wa kwenye daftari la kupigia kura ili
kuweza kupunguza watanzania wengi kukosa haki yao ya msingi na kikatiba kwa kushidwa kufikiwa au upungufu wa vifaa.
Alidai kuwa serikali ingefanya
mapema suala la undikishaji wa daftari la wapiga kura kabla ya Bunge kuvunjwa ili kuweza kuwapa
watanzania nafasi nzuri zaidi ya
kujiandaa uchaguzi mkuu hapo octoba mwaka huu.
Pia amewataka viongozi wa
serikali kujifunza kwa zoezi zima la katiba hii kutokana na kutofanya
maandalizi mazuri kumetokea kuahirishwa ahirishwa kwa zoezi hili kitu
alichosema kinachoashiria ni mapungufu katika maandalizi.
Hata havyo alisema vitendo mbalimbali
vinavyo endelea katika nchi za wezetu
kama Kenya na nchi zingine kwa
watanzania hasa viongozi wote waliopewa madaraka kuweza kuhakikisha wanaitunza amani ,kwa kuvumiliana, kuonyana
,kusameheana kwa kuwa ndio maagizo ya mwenyezi mungu kwa kila aliye na dini na
asiye na dini.
Aliongeza kuwa kumekuwako na
kuteleleka kwa amani, kuteleeka kwa mahusiano katika jamii, na kuteteleka
kwa mahusiano kati ya dini na dini na amesema
tunapopita katika kipindi hiki serikali haina budi kujifunza hayo ili
kuimarisha umoja na amanai ya nchi kwa
kushirikana na jamii,
Aliitaka jamii kila mmoja
aitafute amani na mwenzeke kwa
kuheshimina na kudhaminiana kwa mjibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa
Tanzania.
Alisema nchi yetu anamisingi
madhubuti ya amani serikali isitungize katika mgawanyiko kwa kuishadadia mahakama ya kadhi ya ikizidi
kuinuliwa kwa mlango wa nyuma inaweza
kuvurugika kwa amani katika taifa lisilo kuwa na Dini kama Tanzania
Alisema tanzania haina dini bali
watanzania ndio wenye dini hivyo mahakama ya kadhi isiwe suala la kujadiliwa katika mijadala ya
serikali ili
kupunguza mgawanyiko na uvunjifu wa amani kwa kadri ya waasisi wa taifa letu
laTanzania.
Pia alisema mauwaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi malbino kwa mujibu wa katiba ya Tanzania
inampa kila mmoja haki ya kuishi,pia amedai kuwa kunavitendo
vingine nyuma ya pazia ambapo sasa hata watoto mapacha wanatafutwa kwa imani za kishirikina kwa kile alicho kisema kuwa ni kupngua kwa hofu ya mungu ya ndani ya watanzania .
Comments
Post a Comment