VIONGOZI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUWA VYEO NI DHAMANA.
Na noel Stephen –Mpwapwa
Viongozi wa
umma , viongozi wa kuteuliwa, na viongozi wa kuchaguliwa wilayani mpwapwa wameaswa kuto tumia
dhamana waliyo pewa na wananchi
kama miradi ya ya kujinufaisha
binafsi
Lai hiyo
imetolewa na Kamanda wa kuzuia na kupambana na rushwa
wilayani mpwapwa mkoani Dodoma Michael Makoba
alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mahojianao maluumu.
Makoba amesema
kuwa kumekuwako na kushuka kwa
maadili ya viongozi wa umma ambao
hutumia vyeo vyao kama mitaji ya
kujinufaisha na kuwaacha watu wanaowaongoza wakiwa katika lindi kubwa la
umaskin na kusahau kuwa cheo ni dhamana na kuwatumiakia wananchi
hasa walio katika sekta zao.
Aidha Makoba amedai kuwa
sheria ya ya maadili ya viongozi wa umma na na 13ya
mwaka 1995 sura 398 toleo la 2002 inawahimiza
watumishi wa umma kuboresha nguzo ya utawala bora na uwajibikaji kwa wananchi katika ngazi zote za serikali
hasa ngazi ya serikali za mtaa kwa kuzingatia dhana ya maboresho ya serikali za
mitaa( ugatuzi wa madaraka katika serikali za mitaa.
Ameongza kuwa japo
kuwa serikali imekuwa ikipeleka pesa nyingi katika halmashuri nyingi za wilaya lakini
ndiko kwenye malalamiko mengi ya wanachi na miradi mingi kutekeleza chini ya viwango kitu alichokisema kuwa
kinaashilia mianya ya rushwa na kuto kuwajibika kwa watumishi wa serikali.
Alisema kuwa amani
haiwezi kukuzwa katika nchi yeyote mpaka hapo itakapo kuwa na maadili katika jamii na hasa
kwa kila mmoja
kuwajibika na kutimiza wajibu
wake na wajibu kwa taifa lake na jamii anayo itumikia kwa kuzingatia haki kwa kila mmoja.
Pia amesema kunaonekana dalili za kupungua kwa maadili kwa viongozi
wa umma kwa kushidwa kuvumiliana
katika umoja wa kitaifa na kisiasa, vitu vinavyo tishia amani ya nchi
kwa baadhi ya watumishi
kuendekeza mambo ya kuto
kuwajibika ,rushwa,ubinafsi, na upendeleo.
Amedai kuwa mambo yanayo
endelea nchini kwa kwa baadhi ya
watumishi wa umma kutuhumiwa na kashfa
za rushwa zinakatisha tama wanachi na kupelekea wanachi kuwakatia viongozi wao
walio madarakani na kushidwa kuwachukulia
hatua za kinidhamu.
Mbali na hilo
alisema sekretalieti ya maadili ya viongozi wa umma wamejipanga kuhamisisha jamii kupitia vyombo
ya habari mikutano ya hadahara pamoja na kutumia asasi ziziso kuwa za kiserikali
kuweza kueneza dhana hii kwa wananchi wengi ili waweze kusimamia rasilmali
zao zinazo wazunguka
Kwa upande wake
mchambuzi wa masula ya siasa na jamii mwl Issack Chibwae amesema chanzo cha
kushuka kwa maadili ni baada ya kuanzishwa kwa azimio la
Zanzibar lililo ruhusu kuvunjwa
kwa sheria masharti ya azimio la Arusha la mwaka 1973 kinyume na mtazamo
wa mwasisi wa taifa hili mwl Nyerere.
Alisema sheria hiyo
ilisimamia maadili kwa watumishi wa uuma
na ndio ilikuwa ikisimamia viongozi kuto
jilimbikizia mali na kukataza mtumishi kuwa na mishahara miwili.
Na ameongeza kuwa “baada hapo hali ikawa tofauti na ndo sababu kubwa ya kuanza kuvujika kwa
maadili ya viongozi wa umma na kutufikisha hapa tulipo”alisema Chibwae.
.
Comments
Post a Comment