TASISI YA UTAFITI WA MFUGO YAPATA HASARA MILINI 500 KUTOKA NA MGOGORO WA ARDHI KIBODYANI.
Na stephen noel -
Mpwapwa.
TASISI ya utafiti wa
mifugo TALIRI ilioko wilayani mpwapwa mkoani Dodoma
imepata hasara ya ya zaidi ya
shilingi milioni 500/= kutokana na kuacha kuzalisha mifugo katika shamba lao la
kibodyani kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya tasisi hiyo na wanachi waishio katika
kijiji hicho.
Mkurugenzi wa tasisi
hiyo Dr. Daniel Komuhangilo aliyasema hayo kituoani hapo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari ofisi kwake
juu mgogoro wa a ardhi uliodumu
kwa muda wa miaka mmne sasa tangu
mwaka 2012.
Dr. Komuhangilo alisema
mgogoro huo kila siku zinavyo zidi
kusonga mbele ndipo mgogoro huo
unazidi kuchukua sura mpya na kuzidi kukomaa
na kuhatarishi hata uendelevu wa kituo hicho kwa mstakabaili wa Tanzania na nchi jirani zinazo nufaika na kituo hicho .
Alisema mwaka 2012 kulitokea mgogoro mipaka ya ardhi kati tasisi na wakazi wa
kijiji cha kibodyani na kusababisha baadhi ya watumishi wa kituo walijeruhiwa
na mali za kituo hicho kuharibiwa
ikiwemo gari.
Na alisema shitaka hilo lilifika katika mahakama
ya wilaya ya Mpwapwa na baadhi watuhumiwa walipatikana na hatia na walifugwa kifungo cha miaka mitatu kifungo cha nje.
Alisema alishangazwa
na wanakijiji hicho kuendelea
kuingia kwenye maeneo ya tasisi hiyo ambayo ilikuwa inatumiwa
kama shamba la kuzalishia ng’ombe wa utafiti ambao walikuwa wanazalishwa
na kugawiwa kwa wakulima wa kanda ya kati na Tanzania yote kutokana
ubora wa ngombe waliokuwa katika eneo hilo,
Aidha aliongeza
kuwa kutokana na hali hiyo tasisi hyo
imeshidwa kuzalisha ngombe hao kwa muda wa mika mine sasa ambapo alisema takribani ngombe 800 hawakuzalishwa na tasisi hiyo kutokana na mgogoro huo
ambao kwa sasa unazidi kushika kasi kila kukicha.
Aliongeza kuwa chanzo cha mgogoro huo ni wakazi wa kijiji hicho kuingia kwenye mipaka
ya tasisi hizo na kuanzisha shughuli za
kilimo cha mahindi viazi na mazao mengine kama maharage na
njegere kinyume na utaraibu .
Alisema pia wananchi kutopenda kuheshimu maamuzi ya kisheria
kutokana na kukingiwa vifua na
baadhi ya viongozi hapa nchini
kutapelekea wanachi hao kuudharau mamlaka
ziilizoko kwenye madarakani na
kutapelekea amani kutoweka katika maeneo
mengi hapa nchini.
Pia alisema kuna
baadhi wanasiasa wanahusika kuchochea
mgogoro huo kwa maslahi yao binafsi
ambayo ni kwa ajili ya kupata kura za uchaguzi
kwa mwaka huu 2015.
Alisema amepeleka barua ya tishio la amani katika
kituo hicho kwa mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ambae ni mkuu wa wilaya ya mpwapwa Christopher Kangoye lakini alisema bado hajajabiwa kiofisi tangu
wapelekee barua hiyo.
“Nimeongea nao mala kadhaa
kuhusu suala hilo lakini kila mala nimekuwa nikijibiwa kuwa ebu niache kuwasumbua kwanza
hasa katika mwaka huu wa uchaguzi”Aliongea
Dr. Komuhangilo
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mpwapwa Christopher Kangoye alisema hajapata taarifa za mgogoro huo kuendelea
katika kijiji hicho kutokana na
usuluhishi ulio fanywa na kamati ya
ulinzi na uslama ya wilaya hiyo.
Pia alisema kuwa mkurugenzi huo awasilishe majina ya wanasiasa wanachochoea mgogoro huo kituo cha
polisi kwa hatua zaidi za kisheria “ maana hakuna mtu aliye juu ya sheria juu ya sheria
hatuwezi kuvunja sheria za nchi kwa maslahi ya watu wachache hiyo Tanzania hii inaongozwa kisheria hivyo kila avunjae sheria atachukuliwa
hatua tu”aliongea Kangoye.
Amewataka wananchi
kutii sheria bila shuruti ili
kuweza kudumisha amani katika maeneo ya kazi na sehemu za makazi.
Comments
Post a Comment