WAHUKUMIWA IAKA 20 JELA KWA UNYANG'ANYI



Na Stephen Noel- mpwapwa
 MAHAKAMA  ya wilaya  ya mpwapwa mkoni DODOMA imewahukumu  kifungo cha miaka  ishirini gerezani vijana  watatu wakazi wa Iyoma  wilayani hapa  ambao ni  Ivani Chisomi (36) na Mangaisa  Madelemu(30)  na  Lameck Chikoti28.
Mahakama hiyo iwatia hatiani  vijana  hao baada ya kupataikana na hatia ya unayanaganyi wa kutumia siraha ambapo   waliiba mifugo  aina ya ng’ombe sita   mali ya Mayanda Chikoti.
 Mahakama hiyo ilisema kabala hawajaiba waliweza kumteka  mwenye mali na kupiga na kumjeruhi  na kumweka chini ya ulinzi kwa zaidi ya masaa 9 huku akiwa amefungwa kamaba  miguu na mikono.
Hakimu mkazi mfawidhi  wa mahakama ya wilaya hiyo Jemsi Kareyemaha  alisema  washitakiwa wote watatu  walifanya  kosa  hilo kinyume na viungu 285 na 286 ya kanuni ya adahabu  sura 16 iliyofanyiwa malejeo  mwaka 2002.
“Washitakiwa wote wattu wamepatikana na  hatia  kwa mujibu wa kifungu 286 cha kanuni ya adhabu  no 20 iliyofanyiwa malelejeo mwaka 2002 yanayo wakabili  ya unayangajnyi  wa  kutumia siraha”alieleza  Kareyemaha .
 Kabla ya  mahakama hiyo  haijatoa hukumu  hiyo mwendesha mashitika wa polisi  Michael Joseph  aliiomba  mahakama itoe adahabu kali kwa  washitakiwa wote  iliiwe fundisho kwao na vijana wengine kama wao ambao hawapendi kujishughulisha na kutumia njia za mkatao katika  kutafuta mali na utajiri.
Washitakiwa  kabla ya hukumu waliiomba mahakama iwapunguzie  adhabu kwa maana wanafamilia na watoto wanao wasomesha  na ndugu wengine wanawategemea katika malezi.
Akiwasomea  hukumu  hakimu  Kareyemaha  alisema mahakama  imewatia hatiani hatiani  kwenda kutumika kifungu jela  miaka 20 Ivan  na wenzake  baada ya  kuridhika  na ushahidi na vielelezo  ambavyo  vilivyo tolewa mahakanai  hapo.
Ilidaiwa  kuwa june,  7, mwaka  huu  katika kijiji cha iyoma na mkoa wa Dodoma  Ivan  na wenzake wawili walitenda  kosa  la unyanganyi kinyume na  kifungu 285 na kanuni ya adahabu  no 16 iliyofanyiwa malejeo mwaka 2002.

Comments

  1. Daaa mbayasana hiyo vijana wajifunze waaache tamaaaa wafanye kazi kwa bidiii kubwa sana.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.