RAISI AZITKA HALMASHAURI KUTUMIA VIZURI PESA ZA MFUKO WA BARABARA
Na
Stephen noel- mpwapwa
RAISI wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mlisho Kikwete amezitaka halamashauari zote nchini
kuweza kutunza na kutumia vizuri fedha za ruzuku za
barabara zinazotolewa na serikali ili
ziweze kuondoa kero za barabara vijijini.
Raisi
Jakaya aliyasema hayo katika siku yake ya pili ya ziara mkoani Dodoma wilayani
mpwapwa alipokuwa akiongea na wananchi
wa mpwapwa katika viwanja vya shule ya msingi
Mtejeta.
Dkt Jakaya alisema kuwa serikali imewekeza pesa nyingi sana katika ruzuku ya barabara kwa serikali lakini pesa hizo zimeonekana kuto kuondoa kero ya barabara vijijini kutoka na
baadhi wa watendaji wa halmashauri za
wilaya kushidwa kuzitumia pesa hizo kwa malengo yaliyo kusudiwa bali hujinufaisha wao wenyewe.
Alisema
lengo la serikali ni kuweza kuunganisha
barabara za vijijini ili sehemu
nyingi za vijijini ziweze kufika kirahisi na kurahisha maisha ya watu na kukuza
uchumi kwa kupata faida katika mazao yao
wanayo lima kwa kuyauza kwa bei kubwa inayo
endana na hali ya sasa.
Aidha
Kikwete alisema mwaka 2008 serikali
ilikuwa inawekeza kwenye halmashauri
kiasi cha shilingi billion 55 kufikia mwaka 2012 serikali imekuwa ikiwekeza pesa
kiasi cha shilingi billion 751 amabocho
alisema kuwa nikiasi kikubwa cha pesa
ambacho kinatakiwa kionyeshe
matokeo kwa jamii na kuondoa kero za barabara
vijijini.
“Ikumbukwe
kuwa miaka mitano nyuma serkali ilikuwa inawekeza kiasi cha
shilingi billion 55 kwa halmashauri kwa
ajili ya shughuli za barabra vijijini
hii ni pesa nyingi sana ambazo
tunatamani zionyeshe matokeo kwa jamii lakini halamashauri hizi zimekuwa
zikizitumia vibaya pesa hizi sehemu penye mchwa mingi kwenye
halmashauri pesa hizi haziwezi kuonyesha
matokeo ila pasipo na mchwa pesa hizi zinaweza kuwa ni mkombozi kwa jamii kuhusu masula ya barabara
vijijni.”aliongea Rais
Kuhusiana
na suala la elimu Dkt kiwete
amewataka maafisa elimu na wadau
wa elimu wilayani hapa kuweza kutafuta sababu zinazo pelekea wanafunzi wengi kuweza kuacha shule
njiani kabla ya kufika darasa la saba au kidato cha nne .
Alidai
kuwa kwa mwaka 2007 wanfunzi
waliondikishwa darasa la kwanza walikuwa
wanafunzi 9486 wakati walio fanikiwa kuhitimu darasa la saba walikuwa 6554 ambapo wanafunzi 3430 hawakumaliza darasa la saba
Kwa
kidato cha kwanza mwaka 2010
wanafunzi 2596 waliweza kuanza kidato
cha kwanza lakini walioweza
kuhitimu kidato cha nne walikuwa wanafunzi 1967 ambapo wanafunzi 629 hawakuweza kuhitimu
kidato cha nne, “nawaaagiza maafisa elimu nataka mkae chini mtafute
sababu za hawa wanafunzi kwanini
hawamalizi shule kama wanaolewa basi sheria isimamiwe vizuri akamatwe
aliye oa mwanafunzi afunguliwe mashitaka tunataka huyu mtoto wa kike asome na
asiwe mke wa mtu”alisisitiza Rais.
Akizungumzia
masula ya maabara aliwataka viongozi wa
wilaya hiyo kuongeza nguvu katika ujenzi wa maabara hizo kutokana na kile alicho
kisema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi
wa maabara hizo katika wilaya hiyo amewagiza
viongozi wa wilaya hiyo kumaliza kazi hiyo mapema ifikapo Dec, 2, 2014
na alisema zaidi ya hapo hataitaji maelezo zaidi kutoka kwa kiongozi yeyote.
Kwa
upande wake waziri wa maji Pro.Jumanne
Magembe alisema kutoka na adha ya maji
inayo ikumba mji wa mpwapwa na viunga vyake kutokana na mamlaka ya maji wilayani hapo kushidwa kulipia Ankara za
umeme wanazo diwa na shirika la ugavi
umeme Tanzania TANESCO alisema wizara itailipa tanesco kiasi cha shilingi billion 82 inazo
idai mamlaka ya maji hapa mjini mpwapwa ili kuweza kuimaliza kero ya maji hapa
mjini mpwapwa na kubadilisha mfumo wa mita za ruka katika mashine za maji na
kuweka mita za kawaida.
Pro
Magembe amzitaka tasisi za serikali zinazodaiwa na mamlaka hiyo Ankara za maji kuweza kulipa Ankara hizo mapema iwezekanavyo.
Raisi
kikwete katika ziara yake wilayani mpwapwa aliweza kuweka jiwe la msingi katika
miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa barabara ya
rami inayotoka mbande kongwa na mpwapwa yenye urefu wa km 101 na jenzi
wa daraja la gulwe lenye mita za mraba
70 ilanalo unganisha jimbo la mpwapwa na
jimbo la kibakwe.
Comments
Post a Comment