WAHUKUMIWA IAKA 20 JELA KWA UNYANG'ANYI
Na Stephen Noel- mpwapwa MAHAKAMA ya wilaya ya mpwapwa mkoni DODOMA imewahukumu kifungo cha miaka ishirini gerezani vijana watatu wakazi wa Iyoma wilayani hapa ambao ni Ivani Chisomi (36) na Mangaisa Madelemu(30) na Lameck Chikoti28. Mahakama hiyo iwatia hatiani vijana hao baada ya kupataikana na hatia ya unayanaganyi wa kutumia siraha ambapo waliiba mifugo aina ya ng’ombe sita mali ya Mayanda Chikoti. Mahakama hiyo ilisema kabala hawajaiba waliweza kumteka mwenye mali na kupiga na kumjeruhi na kumweka chini ya ulinzi kwa zaidi ya masaa 9 huku akiwa amefungwa kamaba miguu na mikono. Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya hiyo Jemsi Kareyemaha alisema washitakiwa wote watatu walifanya kosa hilo kinyume na viungu 285 na 286 ya kanuni ya adahabu sura 16 iliyofanyiwa ...