TASISI ZA MKOPO KIKWZO KWA WAJASILIA MALI WADOGO.
Na noel stephen dodoma Tanzania kuna uwezekano mkubwa wa kushidwa kufikia baadhi ya malengo yake milenium kutokana na changamoto zilizoonekana katika utekelezaji wa malengo hayo. Akiongea na radio mwangaza fm mmoja wa wajasilia mali aliyejiatambulisha kwa jina la solomon Ambakisye alisema kuwa kuna chanagamoto kubwa katika kulifikia lengo la tatu la milenium amabalo linadai kuondoa umaskini wa kipato kwa mtanzania . Ambakisye amedai kuwa wajasilia mali wengi nchini hawana elimu ya riba na mikopo kwa tasisi za fedha kitu ambacho kinawapelekea kujingiza kwenye madeni yenye riba kubwa amabayo amesema kuwa badala ya kuwainua kiuchumi bali inazidi kuwadidimiza kwa mikopo hiyo kuwa na riba kubwa. Aidha amedai kuwa bado serikali inatakiwa kulaumiwa kwa hili kutokana na kuweka malengo mengi lakini kushindwa kuiwekea mikakati ya utekelezaji wa malengo hayo. "Tanzania sis...