VYANZO VYA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI
NA NOEL STEPHEN MPWAPWA Imegundulika kuwa migogoro mingi ya ardhi hapa nchini inasababishwa na vijiji vingi kukosa mpango wa matumizi bora ya ardhi. Hali hiyo imegundulika na mwandishi wetu aliyeko wilayani mpwapwa aliyefanya utafiti juu ya kugundua chanzo cha migogoro mingi inayotokea kati ya wafugaji na wakulima inasababishwa na vijiji vingi hapa nchini kuto kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardh. Akiongea mmoja wa maafisa ardhi wilayani mpwapwa Edina Nambua alisema kuwa kwa wilaya ya mpwapwa kuna vijiji tisa tu ambavyo tayari vimefanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kati ya vijiji 124. Aidha Nambua alisema kuwa sababu nyingine inayao pelekea migogoro kati ya wafugaji na wakulima sehemu za vijijini ni baadhi ya watendaji wa ngazi za vijiji na kata kuwa sehemu za kusababisha migogoro hiyo kwa kushidwa kusimamai a sheria no 5 ya ardhi ya mwaka 1999ambayo hupelek...