hali halisi ya stendi ya daladala ya jamatin Dodoma mvua inaponyesha. LICHA ya Manispaa ya Dodoma kukusanya shilingi milioni 163,620,000 kwa mwaka katika kituo cha daladala cha Jamatin, bado kituo hicho kimejaa mashimo na takataka kiasi cha kuwa ni kero kwa wasafiri na kusababisha adha kubwa. Waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo wamejionea uchafu na mashimo makubwa katika kituo hicho huku baadhi ya watu wakielndelea kulalamika kuwa wanapata kero kubwa. Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa daladala mkoani Dodoma(Uwedo), Ibrahimu Mohamed, amesema kituo hicho kina jumla ya daladala 889 na kati ya hizo 20, hiace. Mwenyekiti huyo alisema gari hizo zinakusanya ushuru wa Sh 500 kwa daladala na hiace zinatozwa sh 100 kwa kila siku lakini hawajui fedha hizo zinepelekwa wapi. Mohamed amesema kituo hicho ni kibovu na kinahitaji ukarabati mkubwa lakini tangu mwaka 2003 amekuwa akiufuata uongozi wa Manispaa kuhusu kufanya ukarabati lakini mpaka leo bado wanatoa maji...