KESI YA LULU BADO UPELELEZI
a Lulu bado haujakamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Lakini jana Wakili wa Serikali, Peter Sekwao aliieleza mahakaama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine.Hakimu Mkazi, Agustina Mmbando aliahirisha kesi hiyo na hadi Juni 18, 2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo. Hata hivyo, jana mshtakiwa huyo alilazimika kupandishwa kizimbani mara mbili baada ya tarehe ya kutajwa tena kukosewa. Awali, hakimu Mmbando alisema kuwa kesi hiyo ingetajwa tena Juni 28 kisha mshtakiwa huyo akaondolewa mahakamani na kupelekwa mahabusu akisubiri kurejeshwa mahabusu ya gereza la Segerea. Lakini baadaye alirudishwa tena mahakamani na kupandishwa kizimbani baada ya kubainika kuwa tarehe iliyopangwa ya kutajwa kwa kesi hiyo haikuwa sahihi kwani karani alikuwa amekosea kuhesababu, ndipo ikapangwa Juni 18. Jalada hilo lilipelekwa Mahakama Kuu Ijumaa ya Mei 18, mwaka ...