VIJANA 4800 WAWEZESHWA MITAJI NA SHIRIKA LA BRAC MAENDELEO DODOMA
DODOMA,
Afisa tarafa ya Mpwapwa Bwana Obert Mwalyego akimkabidhi mmoja wa wanufaika wa vifaa vya kufanyia kazi vifaa vya saloon. |
IMEELEZWA
kuwa umaskini wa kipato ni Moja wapo ya yanzo vikuu vya wasichana
wengi kufanyiwa ukatili wa kijinsia ndani ya jamii tunamo ishi.
Kauli
hiyo imetolewa na kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa ambae ni
katibu tarafa wa tarafa ya Mpwapwa Bwana Olbert Mwalyego wakati wa
sherehe za kukabithi vifaa vya kufanyia kazi Kwa Mabinti barehe ambao
walipatiwa mafunzo ya ujasilia Mali na kufuzu mafunzo hayo na shirika la black maendeeo.
Mwalyego amesema Kwa Sasa kundi kubwa linalo jikuta likiathiriwa na masuala ya
ukatili wa kijinsia ni kundi la vijana na
Mabinti barehe ambao wengi wao ambao hawana ajira."ukweli ni kwamba
tafiti mbalimbali zinadai kuwa moja wapo ya vyanzo vya ukatili ni
umaskini wa kipato unaotokana na vijana wengi kukosa mitaji ya kufanyia
kazi hivyo nawapongeza sana Black maendeleo kwa kuwapatia vitendea
kazi mabinti hawa ambapo itapunguza kundi kubwa la vijana waliokuwa hawana ajira" alieleza.
Meneja
wa mradi wa brac maendeleo wilaya ya Mpwapwa Bi Alana Komba amesema kwa
wilaya ya Mpwapwa Mabinti waliohitimu mafunzo hayo Katika nyanja ya
biashara waliwezeshwa vifaa kama Cherehani,vifaa vya saluni,nafaka nguo
za mitumba,vifaa vya kupikia Friji na vitenge .
Naye
meneja wa mradi wa Brac mkoa wa Dodoma Bi Asia Botea amesema mradi ulianza na
Jumla ya washiriki Wasichana/ Wanawake na wavulana 4,800 katika mkoa wa
Dodoma ikijumuisha wilaya ya Dodoma Jiji, Kondoa na Mpwapwa
".washiriki
walio hitimu ni zaidi ya 3800 wengine walishindwa kwa sababu mbalimbali
ikiwemo kuhama makazi, kupata ajira na shughuli zingine za kimaendeleo
na kutotaka kushiriki kwa hiari zao binafsi" alieleza Bi Botea
Mnufaika mwingine wa kata ya Chunyu akikabithiwa cherehani kwa ajili ya kufanyia kazi.
Aidha
amedai kuwa Washiriki zaidi ya 1600 ni wanafunzi walio nufaika kwa
kuwezeshwa vifaa mbalimbali vya kurahisisha kubaki shuleni, vifaa kama
baiskeli kwa wanafunzi wanaosoma mbali, madaftari, mabegi na sweta za
shule kulingana na uhitaji wao ambao alisema vifaa hivyo viliweza kupunguza utoo na kusaidia vijana wengi waliokuwa wakitaka kuacha shule kubaki shuleni.
Hata
hivyo amedai mradi unawezesha wasichana wenye malengo ya kufanya
biashara kwa kuwaongezea au kuwapa mitaji ya biashara wapendazo.
Amesema
lengo la mradi shirika kufanya hivyo ni kuwainua kiuchumi na kuteketeza
umaskini na ukatili wa kiuchumi ambao umekuwa ni wimbi wanalokutana
nalo wasichana na wanawake na kufifisha ndoto zao za kimaendeleo.
"Wasichana
1000 wa Mkoa wa Dodoma wanawezeshwa kwa kupewa vifaa vya Saluni,
cherehani, mifugo, kilimo, nafaka, vitenge, vijora, balo la mitumba na
vifaa vya mapishi ili waweze kujisimamia wenyewe kifedha na kuinuka
kiuchumi."
Ameongeza kuwa kuwawezesha kiuchumi kunaambatana na utoaji wa posho za kujikimu kwa wasichana
waishio mazingira magumu (Kaya fukara) na kuwatafutia masoko Ili kuweza
kuendelea kuwapa elimu za biashara na usimamiaji fedha pamoja na kuwapa
msaada wa haraka pale wanapohitaji kwa lengo la kuhakikisha wanaweza
kuinuka kiuchumi kama lengo mojawapo la mradi.
Amesema zaidi ya Milion 500, zimetumika katika kuhakikisha walengwa wamewezeshwa kwa kiwango bora kulingana na uhitaji wao.
Kwa
upande wake afisa maendeleo ya jamii bwana Bahati Magumula amesema
shughuli zinazofanywa na shirika la black maendeleo zinamgusa Moja Kwa
Moja mwanamke na msichana lakini pia inasaidia sana kupambana na adui
umaskini ambae ni Moja maadui wakuubwa taifa hili tangu tupate uhuru.
Comments
Post a Comment