Posts

Showing posts from 2022

NESI AMBAKA MGONJWA AKIWA WODINI MPWAPWA.

Image
  JESHI la polisi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma limempandisha kizambani Bwana Athuman Kulwa (22) Kwa tuhuma za kumbaka Mgonjwa akiwa wodin. Mtuhumiwa huyo amefikishwa mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nurupedesia Nassary akikabiliwa na kosa la kubaka . Akisomea shitaka lake mwendesha mashitaka wa polisi Bwana William Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyu alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 130kifungu kidogo (1) na cha (2)e na kifungu cha 131 kifungu kidogo (1) cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa malejeo mwaka 2919. Mwita aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kosa Hilo Juni 25 mwaka huu majira ya alfajiri katika wodi ya wogonjwa Katika hospitali ya wilaya ambapo alimbaka Eva Robert (40)Katika hospital ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma. Kwa upande wa mtuhumiwa aliikanusha shitaka lake na mwendesha mashitaka wa polisi aliiambia mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado hivyo mahakaman ipange siku nyingine ya kutajwa. Kesi hiyo namba 109 ya mwaka 2...

SERIKALI YAANZISHA BARAZA LA ARDHI MPWAPWA KUPUNGUZA MIGOGORO..

Image
KUTOKANA na kuwepo Kwa migogoro mingi ya Ardhi Katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Serikali inatarajia kuanzisha Baraza la Ardhi la wilaya ili kuweza kupunguza migogoro hiyo kwa Wakati. Aki zingumza na mwandishi wa habari ofisin kwake kwa mahojiano maluum afisa Ardhi na mali asili wa wilaya hii Anderson Mwamengo amesema kuwa wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zinazo kabiliwa na migogoro mingi ya ardhi inayosababisha baadhi wa watu kuuwana .   Mwamengo amesema kufuatia hali  Serikali kupitia wizara husika inatarajia kuanzisha kwa Baraza la Ardhi kuanzia mwaka mpya wa Fedha "na tayari hatua za awali zimekamilika ikiwemo kuwateuwa wajumbe na mwenyekiti wa Baraza na miundo mbinu ikiwemo Baraza litakapo kuwepo. Alidai Kwa miaka mimwili mfululizo wamesajili zaid ya migogoro mia moja ya ardhi kutoka Katika maeneo tofauti ya wilaya "na migogoro hiyo mingi ilikuwa inasababishwa uelewa mdogo wa jamii juu umiliki pia baadhi ilikuwa inasababishwa na baadhi ya wajumbe wa ...

RAIS SAMIA ANAVYOPAMBANA NA MAADUI WA TAIFA UVCCM MPWAPWA.

Image
  Katibu w a vijana  wilaya ya Mpwapwa Isack Ngongi akiongea na vijana wa kata ya Ng'ambi  hawapo pichani.( Picha na Mpwapwa Habari ) SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO wa Tanzania chini ya Rais wake Samia Suluhu Hassan wameendelea kupambana na maadui watatu wa Taifa hili kwa kuboresha huduma za Jamii zikiwemo Elimu Afya na umaskin wa Kipato. Kauli hiyo hiyo imetolewa na Katibu wa jumuiya ya vijana wilayani Mpwapwa bwana Isack Ngongi alipofanya ziara ya siku moja katika Ng'ambi kuangalia. miradi ya Maendeleo na kuongea na vijana juu uundaji wa vikundi vya ujasilia mali, na ushiriki katika zoez la Sensa litakalo fanyika Agosti 23 mwaka huu. Ngongi amesema viongoz wote kuanzia mwalimu Nyerere wamekuwa wakipigana katika Kuboresha huduma za Jamii "lakini Rais wa awamu ya sita ndio kapiga bao la tiktaka kwa ujenzi wa vituo vya Afya  katika kata nyingi ambapo akina mama wajawazito wanajifungulia karibu, na kusababisha kupungua kwa vi...