WAGOMBEA WAKUMBUSHWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI.
. Mpwap wa . Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiwakumbusha madiwani wa Halmashuri ya Mpwapwa juu ya sheria ya Uchaguzi. Mpwapwa Mkuu wa tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Bi Julieth Mtuy amewatahadharisha wanasiasa wanao taka kuwania nafasi za ubunge na udiwani katika Majimbo ya Mpwapwa na Kibakwe kutojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa kuelekea katika chaguzi mkuu. Mtuy ameyasema hayo na kuwakumbusha wagombea wa vyama vyote kuto jihusisha na vitendo vyovyote vya utaoji wa rushwa kushawishi au kumchafua mgombea mwenzie kama inavyo elekeza sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 kuanzia k ifungu 15,21-23 kinachomtaka mgombea kuweka wazi ghalama za uchaguzi atakazo zitumia ikiwamo misaada zawadi na vitu ingine kama magari na usa...