Madiwani wa wakumbushwa kujaza tamko la mali pindi udiwani unapokoma.
Mpwapwa. Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri yua Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, wamekumbushwa kujaza za maadili na kuwasilisha Matamko ya Mali yao na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma pindi Udiwani wao unapokoma mwezi Julai 2020. Hayo yalisemwa na Afisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw. George Shilla wakati akiwasilisha mada ya Tamko la Mali na Madeni katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halimashauri ya Wilaya ya Mpwapwa juzi. “Jukumu la kujaza fomu ya maadili ni jukumu la kila kiongozi wa umma na halimuhusu mwajiri wake au mkuu wake wa idara hivyo kujaza fomu hizi ni takwa la kisheria ya Maadili namba 13 ya Mwaka 1995 inayomtambua Kiongozi wa Umma binafsi kila mmoja na sio hiyari ya kiongozi” alifafanua bwana Shilla. Aidha Bw. Shilla alidai kuwa Madiwani wana wajibu wao wa kuwasilisha fomu hizo kwa Kamishna wa Maadili wenyewe na siyo...