Mwl.Augusta Lupokela kaimu mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya ualimu ,Wizara ya Elimu Sayansi na Tecknolojia. MBUNGE wa Jimbo la Mpwapwa Mhe George Lubeleje (Seniour MP) ameiomba serikali kuweza kutenga Bajeti ya kutosha katika sekta ya michezo nchini ili kuwezesha kuwezesha tanzania kufanya vizuri katika nyanja ya michezo katika soko la ndani na nje ya michezo na ulimwenguni. Mhe Lubeleje aliyasema hayo juzi alipokuwa akifungua Kongamano la Michezo la vyuo vya ualimu kanda ya kanda linalofanyika katiia chuao cha ualimu kilichopo Mpwapwa Mkoani Dodoma. Mhe Lubeleje alisema kwa sasa nchi ya Tanzania inashidwa kufanya vizuri katika nyanja za michezo kutokana na serikali kushidwa kuwekeza vya kutosha katika sekta hii ya michezo ambayo inaoneka kukua kwa kasi hapa nchini. Aidha amesema kwa sasa soko la michezo hapa nchini limeonekana kushika kasi kubwa na kuwajumuisha vi...
Posts
Showing posts from 2019
AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.
- Get link
- X
- Other Apps
Bwana Odeni Mwikola akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza Maisha Mapya Jela . Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi . Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya. Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya sura 5 ya mwaka 2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa heka moja. Hata hivyo Mayumba aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi. ...
MPINA WAKULIMA BARUA WAKURUGENZI NCHINI,Walioshidwa kukarabati Majosho.
- Get link
- X
- Other Apps
MPWAPWA KITAIFA /KILIMO NA MIFUGO. Waziri wa mifugo na uvuvi bwana Luhaga Mpina amesema anatarajia kuwaandikia barua za kusudio kuacha kukusanya mapato yote yatokanayo na mifugo kwa Halmashauri zilizo shidwa kutekeleza Agizo lake la azimio la Chato la kukarabati Majosho mabovu ili kuongeza huduma za uogeshaji kwa wafugaji. Waziri Mpina ametoa Agizo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipo kuwa kwenye ziara ya kikazi ya kutadhimini zoezi la uogeshaji limefikia Wapi Tangu lizinduliwe mwezi November mwaka 2018. Waziri Mpina amesema Katika uzinduzi huo huko Chato alitoa Maagizo manne kwa Halmashauri zote nchini kuyatekeleza kitu alicho kisema kuwa baadhi ya Halmashauri zimetekeleza na zingine hazijatekeleza. "Nilipokuwa Chato nilitoa maagizo kuwa kila Halmashauri itenge asilimia 15 ya mapato yake ya ndani kwa zitakazo rudi kwa wananchi kuboresha huduma za mifugo nchini. Pia nilisema Majosho yote mabovu yakarabatiwe ili kuongeza fursa za wananchi kuogesha ...