PAROKO KANISA KATOLIKI ATAKA HUDUMA ZA JAMII KUBOREKA MPWAPWA.
Paroko wa kanisa Katoliki Parokia ya Mpwapwa Pd Daud Ngimba akihubiri anisani . PAROKO wa kanisa katoliki Parokia ya Bikira Maria wa Fatima Mpwapwa jimbo kuu la Dodoma Padre Daud Ngimba imeitaka jamii ya watu wa Mpwapwa na viongozi wa Serikali kuweza kutumia fursa ya Serikali kuhamia Mkoani Dodoma kuboresha huduma za kijamii kama , Barabara,shule , Afya na huduma za maji wilayani hapo. Padre Ngimba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipo kuwa akitoa mahubiri kwenye Misa ya Utatu mtakatifu na alipokuwa akiutambulisha mkakati wa kanisa hilo katika kujikita katika utatuzi wa changamoto zinazo ikabili jamii ya Mpwapwa. Padre Ngimba alisema wakristu ,Tasisi za dini pamoja na serikali za mitaa katika mkoa wa Dodoma zitaweza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuhamisha makao makuu ya serikali kuja Dodoma n...