UGONJWA WA NGURUWE WAWATIA UMASKINI WAFUGAJI MPWAPWA.
BAADHI yawafugaji katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameingia hasara kwa kupoteza mifugo yao aina ya nguruwe kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa nguruwe ujulikano kama African swine fever. Wakiongea na Gazeti hili kwa nyakati tofauti mmoja wa wafugaji bi Tabitha Simbeye alisema tangu ugonjwa huo uzuke wafugaji wengi wamepteza nguruwe wengi na hivyo kuwasababishia hasara kubwa. Tabitha alisema katika mtaa wake zidi ya zizi lake kulikuwa na nguruwe sita wote walikubwa na ugonjwa baadhi alifanikiwa kuwauza kwa hasara na wengine walikufa na kuwazika. Alisema nguruwe wengi yameathiliwa na ugonjwa huo ambapo alisema Nguruwe hutetemeka na kukosa nguvu . kushidwa kutembea. Aidha mmoja wa watafiti wa mifugo kutoka katika Tasisi ya utafiti wa mifugo TARILI Mpwapwa ambae jina lake hakutaka liiandikwe alisema kuwa ...