MKINZANO WA SHERIA KIKWAZO UHARIBIFU MAZINGIRA MPWAPWA.
Na Stephen Noel. mpwapwa .
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma
bwana Jabir Shekimweri amesema
mkinzano mkubwa uliopo kati ya sheria mama ya mazingira ya mwaka
2004 na sheria ndogo ya
halmasahauri ya wilaya hiyo ni miongoni mwa sababu zinazo fifisha harakati za kupambana na uharibifu wa
mazingira wilayani hapa.
Shekimweri ameyasema hayo
mjini hapa alipokuwa akifanya mahojiano maluum majira juu ya hakarakati na
mkakati uliopo kwa wilaya ya mpwapwa juu ya uharibifu wa mazingira na matokeo yake.
Shakimweri amesema kuwa sheria ya mama ya mazingira mwaka ya
mwaka 2004 inayo mtaka mharibifu wamazingira anapo patikana na hatia anahukumiwa kifungo cha cha miezi sita hadi mika miwili jela au faini ya
shilingi 50,000/= hadi million 50,000,000/= au vyote viwili kwa
pamoja.
Aidha amesema kuwa sheria
ndogo ya halamasahauri hiyo inayo mtaka mharibifu wa mazingira akipatikana na hatia anatakiwa kulipa faini ya shilingi
50,000/=na isiyo zidi shilingi 300,000/=
hivyo alisema kuwa wengi wao wametumia udhaifu wa sheria ndogo hiyo
kuharibu mazingira na kupelekea wilaya
hiyo kuaanza kukubwa na matokeo ya uharibifu mkubwa wa mazingiara hayo ikiwamo, mafuriko,kukauka
kwa vyanzo vya maji, na upungufu mkubwa
wa mvua unaosababisha Mpwapwa kuwa
katika hatari kubwa ya kukabiliwa na jangwa.
Hata hivyo alisema baadhi ya
makatibu wa kamati za migogoro ya kata wamekuwa wakitumia mwanya wa kesi
za waharifu wa mazingira kuwageuza kama
mitaji ya kuendesha maisha yao kwa kuhongwa kitu kidogo na kuwaaachilia
wakiendelea na uharibifu wa mazingira hayo.
Shekimweri alimtaka
mwanasheria mkuu wa halmasahauri
kuweza kuwashauri madiwani wa halamasahauri hiyo kuweza kuifanyia
malekebisho sheria ndogo hiyo ili iandane na
sheria mama ya mazingira ya mazingira
na hali halisi ya uharibifu kwa wilaya
ya Mpwapwa na matokeo yake.
Comments
Post a Comment