POLISI MPWAPWA YAKABILIWA NA UHABA VITENDEA KAZI.
Na Stephen noel mpwapwa. JESHI la polisi wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma linakabiliwa na upungufu mkubwa wa vityendea kazi ikiwemo magari na pikipiki kitu kinachopelekea jeshi hilo kushidwa kuwahi katika matukio ya kiuharifu. Kauli hiyo ilitolewa jana na Mrakibu wa polisi bwana Paulo Ngonyani mkuu wa kitengo cha Intelinjesia mkoani Dodoma alipokuwa katika hafla ya kukabithiwa Pikipiki mbili zilizonunuliwa na wadau wa polisi wa wilayani Mpwapwa kwa lengo la kupambana na uharifu wilayani hapa. Bwana Ngonyani alisema katika jeshi la polisi limekuwa likilalamikiwa sana na wanajmii kuwa wamekuwa wakichelewa kufika katika matukio ya kiuharifu kutokana na kukabiliwa na chanagamoto kubwa ya ukosefu wa vitendea kazi kama vyombo vya usafiri,pamoja na mafuta Aidha Ngonyani alisema kwamba ili kuimarisha dhana ya polisi jamii wameamua kuwashirikisha wadau wa maendeleo katika wilaya husika...