JUMLA ya watu 94 katika wilaya ya Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma wamegundulika kuumwa ugonjwa wa kipindupindu wakati wawili tayari wamesha fariki Dunia kutokana na ugonjwa huo. Hali hiyo imeelezwa mganga mkuu wa ya wilaya ya Mpwapwa Dkt Siad Mawji alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari juu ya kuwapo kwa wa ugonjwa huo katika wilaya hiyo na kusabaisha hali ya wasiwasi kwa wakazi wengi wa wilaya hiyo na viunga vyake. Dkt Mawji alisema kuwa mgonjwa wa kwanza aligundulika octoba 26 mwaka huu akitokea kata ya Mweznele na wagonjwa wengene waliendelea kujitokeza kutoka katika kata mbalimbali hadi kufikia wagonjwa 94 tangu ugonjwa huo uanze hadi sasa. Hata hivyo alisema w wagonjwa wengine walitokea katika kata ya Tambi,Mpwapwa mjini, Lumuma na Matomondo na kufanya wagonjwa wote kufikia wagonjwa 94. Alion...