SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA KASI ULIPWAJI WA MADAI YA WALIMU.




CHAMA CHA WALIMU (CWT) wilayani Mpwapwa mkoani  Dodoma kimeimeoba Serikali  kuongeza kasi ya ulipwaji wa madai  ya walimu japo kuwa imeonyesha moyo wa kuanza kuyalipa madeni hayo taratibu.
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati ya utendaji  taifa wa chama hicho   bwana Stephen  Maziguni   wilaya ya hapa alipokuwa akiongea  na   walimu na viongozi wa halmasahauri ya  wilaya hiyo  katika kikao cha cha pamoja  cha kujaili changamoto zinazo wakabili  sekta ya elimu  hapa nchini. 
Bwana Stephen  amesema kuwa  serikali imeonyesha moyo wa kulipa madeni ya walimu  lakini yamekuwa yakilipwa  kwa mwendo wa kinyonga kitu walicho sema kunapelekea madeni kuzidi kuongezeka bada la ya kupungua kila mwaka .
Kwa upande wake katibu wa chama  hicho wilayani hapa bwana  Pankras Ngamesha  amesema kati  ya madai mbalimbali  yasiyo kuwa ya mishahara  yasiyolipwa  toka mwaka 2011 – 2016 ni shilingi  million 608,898,126/=.
Ngamesha  amesema  madai  ya malimbikizo  ya mishahara  yaliyolipwa   kwa mwaka  2015- 2016  ni shilingi million 101,660,656.70/=ambayo alisema kiasi kidogo kilicho lipwa ikilinganishwa na kiasi kinachodaiwa hivyo wameiomba serikali kuongeza kasi ya malipo.
Mmoja wa  wa walimu walioshiriki  wa  mkutano huo  Mery Lubuku ametoa malalamiko  kwa viongozi wa halmashauri  ya wilaya Mpwapwa  kuwa wamekuwa wakiwatolea maneno makali walimu hao  na kupelekea walimu hao kukata tama na kushuka kwa kiwango cha Elimu   wilayani hapa.
Kwa upande  wake  kaimu mkurugenzi  mtendaji wa halmasahauri  ya mpwapwa ambae ni ofisa elimu  shule ya Msingi Bi Mery Chakupewa  alisema kuwa halmasahauri hiyo imejipanga kupandisha kiwango cha elimu   wilayani hapa kwa kuboresha  mazingira ya walimu ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi ili Mpwapwa irudi katika viwango vyake  ubora katika ngazi ya kimkoa na kimataifa katika kutoa elimu bora.
Pia amekili kuwepo kwa baadhi  ya watumishi wa halmasahauri  na elimu kuwanyanyasa walimu  kitu alicho kisema tayari wamesha kishughulikia na wengine wamesha chukulia hatua za uhamisho na maonyo.

    

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.