WANASISA NA WATUMISHI WAASWA KUSHIRKIANA KUILETEA JAMII MAENDELEO ENDELEVU.
Na noel Stephen mpwapwa. WATENDAJI na wanasiasa wilayani mpwapwa wanatakiwa kushirikiana katika kuiletea wilaya hiyo maendeleo endelevu. LAI hiyo imetolewa na katibu Tawala wa wilaya hiyo Athanasia Kabuyanja alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari ofisi kwake mapema wiki kwa mahojianao maluumu. Kabuyanja aliwataka watumishi na watendaji wa serikali kuweza kushirikiana katika kuiletea wilaya hiyo maendeleo endelevu juu juu kilimo, utunzaji mazingira, utawala bora na huduma za jamii ili mtanzania aifurahie nchi yake na anufaike na kodi anazo lipa. ALISEMA kwa wilaya ya mpwapwa ni miongoni mwa wilaya amabazo ziliweza kuingia katika migogoro ya kiutendaji kati wa watumishi na wanasiasa kwa mwaka 2013 kitu alicho kisema kuwa kwa sasa hali hiyo imetulia na ushirikiano umemalika. Aidha alisema ...