AUWA MKEWE KWA KIPIGO
Na noel Stephen mpwapwa.
JESHI la polisi wilayani mpwapwa Kijana mmoja aliyefahamika
kwa jina la Hamis Nwage kwa tuhuma za kupiga hadi kumuua mke (mpenzi
wake).
Tukio hili
lililotokea asubuhi ya feb 11 katika
eneo la hazina wilayani mpwapwa mkoani
Dodoma ambapo kijana huyo alimpiga hadi kumuua mke wake aliyetambulika
kwa jina Amana Makamba kwa kutumia kitu kianachosadikiwa kuwa ni kizito hali
iliyosababisha mauti(37) .
Akiongea mmoja wa
mashuuhuda wa tukio hilo ambae ni dada wa marehemu Bi
Stela Mwasongwe amesema
kuwa siku ya tukio walikuja kuambiwa na majirani
kuwa mdogo wake anasadikiwa kuwa
kapigwa na kujeruhiwa na mume
wake ndipo walipofika eneo hilo na kumkuta mdogo wake huyo akiwa
amekwishafariki.
Mjomba wa marehemu musa
mhina amesema kuwa hajui kilichotokea juu ya mtoto wao bali
walikuja kuambiwa asubuhi ya leo
kuwa mtoto wao ameuwawa na mumewe kwa tuhuma za wivu wa mapenzi .
AIDHA amedai kuwa
tangu kuanza kwa mapenzi yao wao
kama wazazi walimkataza binti yao kuolewa na
bwana huyo kutokana na kuwa bwana huyo
hutumia madawa ya kulevya sana .
Mara baada ya kufanyia kitendo hicho cha mauaji mtuhumiwa
alikunywa maji ya betri kwa lengo la kujiua lakini wasamaria wema walimuwahisha
hospitali ya wilaya ya mpwapwa kkwa matibabu.
Kamanda wa polisi wilayani mpwapwa amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea juu ya tukio hilo.
Comments
Post a Comment