Na noel stephen mpwapwa. Hakimu mkazi Adrikian Kilimi wa Mahakama ya wilaya mpwapwa imewahukumu kwenda jela miaka mitatu bwana Patric Mwidowe,Sehewa Chitema, na Kedmon Chitema wakazi wa kijiji cha kiboroani wilayani mpwapwa mkoani Dodoma kwa makosa ya kuvamia na kuharibu mali na kuchoma mali za Tasisi ya utafiti wa mifugo TALIRI . Akieliza mbele mbele ya mahakama hayo wakili wa serikali Godfrey Wamabali alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa walilifanya kosa hilo December 19,mwaka huu katika maeneo ya kijiji cha kiboriani wilayani mpwapwa mkoani Dodoma wakiwa wote kwa pamoja, Kesi hiyo iliyokuwa ikiwa kabili wakazi wa Kijiji cha Kiboriani kata ya mpwapwamjini wilayani mpwapwa mkoani Dodoma iiliyowahusisha wanakijiji wa kijiji hicho hatimae ilifikia kikomo chake baada ya mahakama kuwahukumu washtakiwa kwenda jela miaka mitatu ...