TAKUKURU WAJA NA MBINU MPYA ZA MAPAMBANO YA RUSHWA.
Mpwapwa Uongozi wa Kata ya Mima na mkuu wa TAKUKURU WA pili kulia wakiwa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Mima. WANANCHI wa kata ya Mima mkoa wa Dodoma wameipongeza Tasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani Mpwapwa kwa kuanzisha mpango wa kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kusikiliza kero zao zinaohusiana na masuala ya Rushwa na Utawala bora. Mmmoja wa wananchi wa kata hiyo bwana Mathias Cosmas ametoa pongezi kwa uongozi wa TAKUKURU wilayani hapa katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi katika kta ya Mima. Bwana Cosmas amesema mara nyingi wananchi wanakuwa nakero zao za kuhusiana na uongozi rushwa na utawala bora lakini wanashidwa kuzitoa kutokana na umbali au kuto kujua taratibu za njisi ya kuwasilisha malalamiko hayo. Bwana Mathias amedai kuwa hatua hiyo itasaidaia Tasisi kupata taarifa nyingi kwa wakati ...