WANANCHI IGOVU WAHAMASISHANA KUFANYA MAENDELEO
Na Stephen Noel. Wananchi wa Mtaa wa Igovu kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa mtaa baada ya kumaliza shughuli za maendeleo. WANANCHI wa Mtaa wa Igovu kata ya Mpwapwa mjini Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameushauri uongozi wa serikali za mitaa ngazi ya halmashauri kuweza kushirikiana na uongozi ngazi ya mitaa kutumia rasimali walizonazo kuondoa chanagamoto ndogondogo zinazowakabili wananchi kuliko kutegemea bajeti ya serikali kuu. Wananchi hao walitoa ushauri huo walipokuwa wakiongea na mwandishi wa habari jana walipokuwa katika shughuli za maendeleo za mtaa wa Igovu kwa kuchimba barabara na kuweka kufusi ili kuweza kurahisisha upitakaji wa njia mtaani hapo. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo bwana Elieza Mwaluko alisema kwa sasa seikali ina miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa “lakini serikali ngazi ya halmashauri na serikali za mit...