AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIKA 30 JELA KWA KOSA LA KULIMA BANGI.
Bwana Odeni Mwikola akiwa chini ya ulinzi wa Polisi akisindikizwa kwenda kuanza Maisha Mapya Jela . Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu kifungo cha miaka thelani jela bwana Oden Mwikola (32) baada ya kupatikana na hatia ya kulima zao haramu la Bangi . Kesi Hizo zilizo kuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya. Hakimu mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Oden Mwikola alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(a)na(b)ya kuzuia madawa ya kulevya sura 5 ya mwaka 2015 ambapo walilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa heka moja. Hata hivyo Mayumba aliiambia Mahakama kuwa kesi hiyo iliyopewa nguvu na mashahidi 5 na vielelezo vitatu ikiwemo hati ya ukamataji, maelezo ya onto na taarifa ya mkemia mkuu iliyo thibitisha kuwa mmea ulio patikana Katika shamba la Bwana Odeni ilikuwa ni Bangi. ...