LUFU WAPATA BARABARA TANGU UHURU.
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma imewataka wakazi wa kata za Mwanawota na Lufu waliopatiwa fedha za ukarabati wa barabara kuthaminisha ukabarabati wa barabara hizo sambamba na uboereshaji uchumi wa kata zao kwa kufanya kazi kwa Bidii. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri alipotembelea barabara hizo kwa ajili ya kuangalia hali halisi ya ukarabati unaoendelea katika kata hizo chiniya wakala wa barabara Vijijini TARURA Wilaya ya Mpwapwa. Barabara zilipatiwa fedha za ukarabati ni barabara ya kibakwe ,Mwanawota yenye urefu wa kilometa 16 yenye dhamani ya shilingi shilingi milion 713,000,000/= na barabara ya kata ya Rufu yenye urefu wa kilometa kilometa 16 pia Shekimweri alisema hakuna zaidi kwa kata hizi kutoa shukrani kwa serikali ya awamu ya tano zaidi ya kupandisha kiwango cha uchumi katika kata zao ambazo zimepatiwa fedha za ukarabati. “...