JAMII YAFICHA TAARIFA ZA UKATILI.
MTANDAO wa polisi wanawake wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umesema kasi ya ukatili kwa watoto inasababishwa na jamii kuficha taarifa za vitendo hivyo. Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa dawati lá njisia katika kituo cha polisi wilayani hapa Bi Elfrida Mapunda katika maadhimisho ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa dawati hilo. Bi Mapunda amesema kuwa vitendo vya ukatili vinavyodhidi kushika kasi vinasababishwa na jamii kuzidi kuvifumbia macho vitendo hivyo au kamalizana kienyeji bila kufuata sheria na bila kuangalia madhara. Aidha Bi Mapunda ameitaka jamii kwa kusaidiana na jeshi lá polisi kuweza kushirikiana katika kukomesha vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake. Pia amesema katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao huo kumeongezeka kwa taarifa za ukatili ambazo hapo awali zilikuwa zinafichwa kutolewa. Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi Selina Chimwaga amesema kuwa kuwa kundi kubwa lá watoto hao wenye mtindio wa ubongo wanakabiliwa na chan...