ASKOFU KINYAIA AWAASA WATANZANIA.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dodoma Mhasahamu askofu Beatus Kinyaia amewataka watanzania kuto kukubali kufa kizembe kwa kungangania mazoea ya kuto kupanda mazao yanayostahimili ukame katika kipondi hiki cha mabadiliko ya Tabia ya hali ya hewa. Askofu alizungumza hayo jana jumapili ya januari Mosi 2017wakati wa misa katika Kanisa la Bikira maria wa Fatima kanisa la hija katika Parikia ya Mpwapwa . Kinyaia amesema haridhishwi na tabia ya baadhi ya watanzania wengi kuendelea kung’ang’ania mazoea ya kuto kukabiliana na ushauri wa watalaam na maafisa kilimo kuwataka kupanda mazao yanayoweza kukomaa mapema na yanayoweza kustahimili ukame ili kuweza kupata tija ya kilimo chao Aidha Askofu Kinyaia alisema “siku za hivi karibuni mamlaka ya ya utabili wa hali ya hewa imetangaza kuwa katika kipindi hiki cha msimu wa mv...