VIONGOZI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUWA VYEO NI DHAMANA.
Na noel Stephen –Mpwapwa Viongozi wa umma , viongozi wa kuteuliwa, na viongozi wa kuchaguliwa wilayani mpwapwa wameaswa kuto tumia dhamana waliyo pewa na wananchi kama miradi ya ya kujinufaisha binafsi Lai hiyo imetolewa na Kamanda wa kuzuia na kupambana na rushwa wilayani mpwapwa mkoani Dodoma Michael Makoba alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mahojianao maluumu. Makoba amesema kuwa kumekuwako na kushuka kwa maadili ya viongozi wa umma ambao hutumia vyeo vyao kama mitaji ya kujinufaisha na kuwaacha watu wanaowaongoza wakiwa katika lindi kubwa la umaskin na kusahau kuwa cheo ni dhamana na kuwatumiakia wananchi hasa walio katika sekta zao. Aidha Makoba amedai kuwa sheria ya ya maadili ya viongozi wa umma na na 13ya mwaka 1995 sura 398 ...