Posts

Showing posts from October, 2023

KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.

Image
 Mpwapwa. Habari. Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo  akiongea kwenye mkutano kazi wa RUWASA na wadau wa maji uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya.(picha na Emanuel Uronu(Vaino) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma Bi Sophia Kizigo  amezitaka jumuiya za watumia maji  kuweza kuunganisha nguvu  za jumuiya moja na nyingine ili kuweza kutoa huduma   bora  kwa wananchi. Kizigo ametoa Rai  hiyo wakati wa kikao kazi cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya mjini hapa   kilicho wajumuisha  Viongozi wa jumuiya za watumia maji  watendaji wa kata na vijiji napamoja na  madiwani wa kata husika , Kizigo amesema pamoja na serikali ya awamu ya sita kuweka dhamira thabiti ya kumtua  mama ndoo kichwani  lakini bado  jamii husika imeendelea   na uharibifu wa mazingira unaotishia uendelevu wa miradi mikubwa ya maji  inayowekezwa na serikali. Kupitia changamoto hiyo...