DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo akifungua kikao cha wadau wa Ulinzi dhidi ya Mtoto na ukatili wa kijinsia kilicho wezeshwa na Jukwaa la utu wa Mtoto CDF wilayani Mpwapwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akichangia jambo katika kikao cha kujadili ulinzi wa Mtoto wilayani Mpwapwa. Stephen Noel-Mpwapwa. Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Sophia Mfaume Kizigo ametoa amri kwa maafisa Elimu wote ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha shule zote za Msingi na sekondari zinakuwa na walimu walezi kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto wawapo shuleni. Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa Siku moja uliondaliwa na Asasi ya kiraia jukwaa la utu wa mtoto CDF iliyo kutanisha Wadau wote wanao fanya afua za kumlinda mtoto na kujali ustawi wa mtoto. Amesema Ili kuhakikisha watoto wanakuwa Kwenye mazingira ya usalama lazima kunakuwapo na watu w...