UMOJA WA WANAWAKE MPWAPWA WASAIDIA MADAWATI SHULE YA MSINGI VIGH'AWE .
Kamati ya maandalizi ya Umoja wa wanawake Wilaya ya Mpwapwa wakimuonyesha Mgeni Rasmi moja ya dawati walilo tengeneza kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Vigh'awe waliokuwa wakisoma huku wakiwa wanakaa chini kwenye Sakafu. Mgeni Rsmi Bwana Leo Mzeru katika kwenye sherehe ya maombi ya wanawake wa Kikiristo Mpwapwa. Maandamo ya wanawake katika viunga vya mji wa Mpwapwa kwenye sherehe za siku ya mwanamke Duniani, Na Stephen Noel- MPWAPWA WANAWAKE WASAIDIA WANAFUNZI WALIOKUWA WAKISOMA HUKU WAMEKAA CHIN I Wanawake wakikiristu wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameeaswa kuwa pamoja na kupambana na changamoto za kujikwamua kiuchumi laknini wasisashau majukumu yao ya kijinsia kama kulea na kunyonyesha watoto. Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Nowadia zaidi kwenye mahubiri yake alipokuwa akiwahubiria akina wanawake kwenye sherehe za maombi ya umoja wa wananwake wa wakristu Mpwapwa iliyofanyika katika kanisa la watakatifu...