DC MPWAPWA AMESEMA HAKUNA MTU ATAKAYE KUFA KWA COVID 19KAMA WATAZINGATIA MAELEKEZO YA WATAALAM.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bwana Jabir Shekimweri Akiongea na Mwandishi wa habari hizi ofisi kwake. Picha na Mpwapwa Habari. Na Stephen Noel . Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Bwana Jabiri Shekimweri amesema wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA CIVID- 19 na wasitishwe na mamneno ya mitandao juu ya ugonjwa huo. Mkuu wa wilaya ameyasema hayo jana ofisi kwake akifanya mahojiani na na mwandishi wetu juu ya mkakati wa wilaya thidi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ambao kwa sasa umekuwa ni janga la kimataifa. Shekimweri amesema lazima wananchi waelewe na kuendelea kuchukua tahadhari thidi ya ugonjwa huo ambapo kama “ kama wilaya tayari tumesha fanya uhamasishaji katika makundi yote yanayo tuzunguka wakiwemo wafanya biasahara bodaboda masokoni makanisani na misikiti juu ya kujenga uelewa kwa jamii na njia za kujinga ...