Posts

Showing posts from December, 2017

MAJI KIKWAZO CHA MAENDELEO IDILO WILAYA YA MPWAPWA

New post el-Mpwapwa Wakazi  wa kijiji cha Idilo kata ya Mazae wilayani  Mpwapwa mkoani hutumia maji yasiyo salama  na kutishia kupata magonjwa ya mlipuko hasa kipindi hiki kuelekea msimu huu wa mvua za vuli. Maji hayo yanayopatika  umbali km 2 hadi 3 kwa  pia ni maji ya makorongoni ambayo  ni hatari kwa afya za wakazi hao. Diwani wa kata hiyo  bwana Wiliam Vahae   amesema  wakazi hao hulazimika kuamka alfajili na mapema ili kuwahi maji katika kisima kabla hayajachafuliwa na wanyama  wa polini lakini kabla ya wafugaji hawajanza kunywesha  Ng,ombe ambao wanakuwa na makundi makubwa ya mifugo. Aidha Vahae amesema kutokana na hali hiyo  kumepelekea wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya visima vya asili na makorongo ambayo si safi na salama na kutishia magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi. Amesema kufutia tatizo hilo tayari wakazi wa kijiji hicho wamesha changa kiasi cha shilingi million 450,000/=ambazo ...