SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA KASI ULIPWAJI WA MADAI YA WALIMU.
CHAMA CHA WALIMU (CWT) wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kimeimeoba Serikali kuongeza kasi ya ulipwaji wa madai ya walimu japo kuwa imeonyesha moyo wa kuanza kuyalipa madeni hayo taratibu. Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati ya utendaji taifa wa chama hicho bwana Stephen Maziguni wilaya ya hapa alipokuwa akiongea na walimu na viongozi wa halmasahauri ya wilaya hiyo katika kikao cha cha pamoja cha kujaili changamoto zinazo wakabili sekta ya elimu hapa nchini. Bwana Stephen amesema kuwa serikali imeonyesha moyo wa kulipa madeni ya walimu lakini yamekuwa yakilipwa kwa mwendo wa kinyonga kitu walicho sema kunapelekea madeni kuzidi kuongezeka bada la ya kupungua kila mwaka . Kwa upande wake katibu wa chama hicho wilayani hapa bwana Pankras Ngamesha amesema kati ya madai mbalimbali yasiyo ku...