KIJANA WA MIAKA 20 ABAKA MTOTO WA MIAKA 6 PWAGA MPWAPWA
Na noel Stephen mpwapwa Kijana mmoja aliye tambulika kwa jina Teophil Nganga(20)mkazi wa kijiji cha Pwaga wilayani mpwapwa mkoani Dodoma anashikiliwa na polisi katika kituo cha polisi Kibakwe kwa tuhuma za kutaka kumbaka mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa chekekaea katika shule moja wapo ya kata hiyo. Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika kata ya Lumuma wilayani mpwapwa ambapo kijana Teophil anadaiwa kumbaka mtoto huyo kwa kumdanganya kwa kutaka kumpa karanga za kutafuna. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo na mwanaharakati wa shirika la AFNET la kuapmabana na vtendo vya ukatili wa kijinsia katika kata hiyo Clemenc Ngewe aliambia mwananchi kuwa kijana huyo alimwita mtoto huyo kwa madai ya kutaka kumpa karanga na ndipo alipo mwingiza ndani ya chumba chake na kuanza kumbaka. Clemenc al...