*VIJANA WA BBT – LIFE WAONESHWA VITALU,RAIS SAMIA ATAJWA KWA MCHANGO WAKE MKUBWA KWENYE SEKTA YA MIFUGO*
Na Stephen Noel Kagera. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka historia ya kutafsiri ndoto halisi ya wingi wa mifugo nchini katika kubadilisha mfumo wa maisha kwa watanzania kupitia sekta hiyo. Akizungumza (21.05.2024) wakati wa hafla fupi ya kuwaonesha vijana wanaohitimu mafunzo ya unenepeshaji mifugo kupitia Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT – LIFE), inayosimamiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, vitalu watakavyopatiwa kwa ajili ya ufugaji katika Ranchi za Kagoma na Kitengule zinazosimamaiwa na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mhe. Julius Laizer amesema Mhe. Rais ameweza kuirasimisha rasmi biashara ya mazao ya mifugo kwa kuwa Sekta ya Mifugo ni muhimu katika maisha ya binadamu. Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Ranchi ya Kagoma iliyopo Wilaya ya Karagwe mkoani humo ya kuwaonesha vijana wanaohitimu mafunzo ya unenepeshaji mifugo kupitia Programu ya Je...