Posts

Showing posts from January, 2017

ASKOFU KINYAIA AWAASA WATANZANIA.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dodoma Mhasahamu askofu Beatus Kinyaia   amewataka watanzania kuto kukubali kufa kizembe kwa kungangania   mazoea   ya kuto kupanda mazao yanayostahimili ukame katika kipondi hiki cha mabadiliko ya Tabia ya hali ya hewa. Askofu   alizungumza   hayo jana   jumapili ya januari Mosi 2017wakati   wa misa katika   Kanisa la Bikira   maria   wa Fatima kanisa la hija   katika Parikia ya Mpwapwa . Kinyaia   amesema haridhishwi na tabia ya baadhi ya watanzania wengi   kuendelea kung’ang’ania   mazoea ya kuto kukabiliana na ushauri wa watalaam na maafisa kilimo kuwataka kupanda mazao yanayoweza kukomaa mapema   na yanayoweza kustahimili ukame   ili kuweza kupata tija ya kilimo chao Aidha Askofu   Kinyaia   alisema “siku za hivi karibuni   mamlaka ya   ya utabili wa hali ya hewa imetangaza kuwa katika kipindi hiki cha   msimu wa mvua kutakuwa na mvua chini ya wastani hivyo kuwataka wananchi kuweza kupanda mazao yanaweza kuhimili ukam

Mpango wa PWP TASSAF MPWAPWA UTASAIDIAMAZINGIRA

Imeelezwa    kuwa    shughuli za   ajira muda zilizofanywa na walegwa wa mpango wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu kama kutunza Misitu ya asili,uvunaji wa maji ya mvua, na utunzaji wa udongo,ikitumika inavyopaswa itaweza kuleta mabadiliko   chanya kwa   jamii   na kuweza kujiletea maendeleo endelevu. Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa Tassaf wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Paskal Jeremia   alipokuwa akiongea   na waandishi wa habari ofisini kwake juu tadhimini   ya utekelezaji wa mpango wa ajira za muda zijulikanozo kama (PWP)kwa wanufaika wa mpango huo wilayani hapa Jeremia alisema   rasilimali hizo kama ujengaji wa miundo mbinu ya   kuvuna maji ya mvua, wa   utunzaji wa misitu, na   uhifadhi wa   udongo   ngazi ya jamii italeta mabadiliko   kuwa   mazuri   zaidi   na jamii kuweza kujiletea   maendelea endelevu katika maeneo yao yanayoishi . Aidha   alisema kwa sasa zoezi hilo limetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 70% katika vijiji vyote   ambavyo   mradi huo u