Posts

Showing posts from July, 2016

SERIKALI YAOMBWA KUONGEZA KASI ULIPWAJI WA MADAI YA WALIMU.

CHAMA CHA WALIMU (CWT) wilayani Mpwapwa mkoani   Dodoma kimeimeoba Serikali   kuongeza kasi ya ulipwaji wa madai   ya walimu japo kuwa imeonyesha moyo wa kuanza kuyalipa madeni hayo taratibu. Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa kamati ya utendaji   taifa wa chama hicho     bwana Stephen   Maziguni     wilaya ya hapa alipokuwa akiongea   na     walimu na viongozi wa halmasahauri ya   wilaya hiyo   katika kikao cha cha pamoja   cha kujaili changamoto zinazo wakabili   sekta ya elimu   hapa nchini.   Bwana Stephen   amesema kuwa   serikali imeonyesha moyo wa kulipa madeni ya walimu   lakini yamekuwa yakilipwa   kwa mwendo wa kinyonga kitu walicho sema kunapelekea madeni kuzidi kuongezeka bada la ya kupungua kila mwaka . Kwa upande wake katibu wa chama   hicho wilayani hapa bwana   Pankras Ngamesha   amesema kati   ya madai mbalimbali   yasiyo kuwa ya mishahara   yasiyolipwa   toka mwaka 2011 – 2016 ni shilingi   million 608,898,126/=. Ngamesha   amesema   madai   ya malimbik