Posts

Showing posts from February, 2015

VIONGOZI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUWA VYEO NI DHAMANA.

  Na noel Stephen –Mpwapwa   Viongozi wa   umma , viongozi wa   kuteuliwa,   na viongozi wa kuchaguliwa   wilayani mpwapwa wameaswa    kuto tumia   dhamana waliyo pewa na wananchi   kama miradi ya   ya kujinufaisha binafsi Lai hiyo imetolewa   na    Kamanda wa kuzuia na kupambana na rushwa wilayani mpwapwa mkoani Dodoma Michael Makoba   alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari kwa mahojianao maluumu. Makoba   amesema   kuwa kumekuwako na   kushuka kwa maadili ya viongozi wa umma   ambao hutumia   vyeo vyao kama mitaji ya kujinufaisha na kuwaacha watu wanaowaongoza wakiwa katika lindi kubwa la umaskin na   kusahau kuwa   cheo ni dhamana na kuwatumiakia wananchi hasa   walio katika   sekta zao. Aidha   Makoba   amedai kuwa    sheria ya   ya maadili   ya viongozi wa umma   na   na 13ya mwaka 1995 sura 398   toleo la 2002 inawahimiza watumishi wa umma kuboresha nguzo ya utawala bora na uwajibikaji   kwa wananchi katika ngazi zote za serikali hasa ngazi ya serikali z

TASISI YA UTAFITI WA MFUGO YAPATA HASARA MILINI 500 KUTOKA NA MGOGORO WA ARDHI KIBODYANI.

Na stephen noel   - Mpwapwa. TASISI   ya utafiti wa mifugo   TALIRI   ilioko wilayani mpwapwa   mkoani Dodoma   imepata hasara ya   ya zaidi ya shilingi   milioni 500/= kutokana na   kuacha kuzalisha mifugo katika shamba lao la kibodyani   kutokana na mgogoro wa ardhi   kati ya tasisi hiyo na wanachi waishio katika kijiji hicho. Mkurugenzi   wa tasisi hiyo   Dr. Daniel Komuhangilo   aliyasema hayo kituoani hapo alipokuwa akiongea na waandishi   wa habari   ofisi kwake   juu mgogoro wa a ardhi uliodumu   kwa muda wa miaka mmne sasa   tangu mwaka    2012. Dr. Komuhangilo alisema   mgogoro huo kila siku zinavyo zidi   kusonga mbele ndipo   mgogoro huo unazidi kuchukua sura mpya na kuzidi kukomaa   na kuhatarishi hata uendelevu wa kituo hicho   kwa mstakabaili   wa Tanzania na nchi jirani   zinazo nufaika na kituo hicho . Alisema mwaka 2012 kulitokea mgogoro   mipaka ya ardhi kati tasisi na wakazi wa kijiji cha kibodyani na kusababisha baadhi ya watumishi wa kituo walijeruhiw